 
 
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Akizungumza hivi
 karibuni, Gwajima alisema tukio hilo lilijiri nyumbani kwake, Mbezi 
Beach jijini Dar ambapo siku ya kwanza, majambazi hao waliingia nyumbani
 kwake saa nne usiku wakiwa wameficha sura na kumkuta yeye sebuleni 
ambapo walimuuliza, ‘Gwajima yuko wapi?’
“Ni kweli nilinusurika kifo na majambazi, walinivamia mara tatu nyumbani. 
Zilikuwa
 siku mbaya maishani mwangu. Siku ya kwanza walikuja na bunduki huku 
wameficha sura, walinikuta sebuleni, wakaniuliza alipo Gwajima, 
niliwajibu ametoka, wakaondoka wakisema watarudi kesho yake.
“Nilijua
 ni utani, lakini kweli siku iliyofuata saa nne usiku walikuja tena, 
wakanikuta ndiyo naingia nyumbani, wakaniambia niko chini ya ulinzi, 
nilimuomba Mungu aokoe maisha yangu kwani nilipatwa na mshtuko, 
wakahoji; ‘Gwajuma yuko wapi?’ Kabla sijajibu mmoja akasema; ‘huyu bwana
 mdogo ndiye tuliyemkuta jana,’ wakaondoka.
“Sikuwa
 na wazo la kuripoti polisi ila nilimwamini Mungu aliye hai. Siku ya 
tatu walipitia juu ya paa kwa kung’oa vigae na kushukia chumbani wakiwa 
na bunduki.
“Mimi
 nilikuwa kitandani na mke wangu, wakauliza tena Gwajima yuko wapi? 
Nikawajibu bado hajarudi, wakasema; ‘haka (Gwajima) ndiyo kale kale ka 
bwana mdogo ka jana.’
“Mungu mkubwa, kwa nje zilisikika kelele za mbwa kisha wakatoweka ghafla, niliona ni siku za majaribu kwangu, nilimwomba Mungu atupilie mbali majaribu yale, baada ya siku kadhaa niliamua kuhama kwenye nyumba ile.
“Ila nakumbuka ile siku ya mwisho walisema tunamtaka Gwajima kwa sababu anajifanya kufufua misukule kisha anataja majina yetu.
“Ndipo
 nilijua kumbe kisa ni kufufua misukule. Najua umbo langu ndiyo mkombozi
 wa yote kwani waliponiona walijua Gwajima hawezi kuwa na umbo dogo kama
 mimi nilivyo,” alisema Gwajima.
Katika mahojiano marefu na Paparazi wetu, mchungaji huyo alisema kuwa mpango wa kumuua uliofanywa na mtu ambaye aliwahi kutajwa jina na binti msukule aliyemfufua kanisani kwake. Alisema mtu huyo aliyetajwa na msukule ni mtumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (jina hakumtaja).


 
 
 
 
 
 
