MAMA wa marehemu Steven Kanumba, Frola
Mtegoa ameibuka na kueleza kuwa, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni mkwe
sahihi kwake kwa namna alivyo na heshima na anavyomjali kama mama yake.
Mama mzazi wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa akipozi na Lulu.
Akizungumza wikiendi iliyopita nyumbani
kwake, Kimara - Temboni, Dar, mama huyo alisema, kama mwanaye angekuwa
hai angekuwa amepata mke bora wa maisha yake, naye pia alikuwa na mkwe
sahihi.
“Najua mtoto wangu ametangulia mbele za
haki lakini faraja anayonipa Lulu ni kubwa mno na najisikia furaha.
Kama Mungu angemwacha Kanumba hai mpaka leo kwa kweli Lulu angekuwa
mkwe bora sana kwangu.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Sina jinsi, ndiyo imeshatokea lakini
mimi kama mzazi bado nitaendelea kumpenda na kuwa bega kwa bega na Lulu
hata akipata mchumba mwema wa kumuoa, sina tatizo na hilo... namwombea
sana kwa Mungu huyu binti,” alisema kwa hisia mama Kanumba.