Jambo limezua jambo! Mvua zilizonyesha na kusababisha mafuriko maeneo
ya Dumila mkoani hapa, zimemuumbua mke wa mtu ambaye jina lake
halikupatikana, akiwa anasaliti ndoa gesti.
Mafuriko hayo yalisababishwa na mvua kubwa zilizoanza kunyesha Jumatano iliyopita na kusababisha maafa makubwa yakiwamo kuharibiwa kwa makazi ya watu, majengo ya serikali zikiwamo shule, vyuo na mahakama.
Mafuriko hayo yalisababishwa na mvua kubwa zilizoanza kunyesha Jumatano iliyopita na kusababisha maafa makubwa yakiwamo kuharibiwa kwa makazi ya watu, majengo ya serikali zikiwamo shule, vyuo na mahakama.
Shuhuda
wa tukio hilo, Lugendo Seleman, mkazi wa Kijiji cha Magole Tarafa ya
Dumila Wilaya ya Kilosa mkoani hapa alimuonyesha mwandishi wetu gesti
ambayo jamaa aliyefahamika kwa jina moja la Kashinde, mkazi wa kijiji
hicho ambaye alikurupuka kuokoa maisha yake akiwa na mke wa mtu.
“Za
mwizi kweli 40, Kashinde katoka gesti uchi wa mnyama na kupiga mbizi
akiwa na mke wa mtu ambaye mumewe amesafiri muda mrefu yuko mjini
akisaka maisha na ana kama miezi 6, huwa anakuja na kuondoa hivyo mkewe
amekuwa na uhuru,” alisema Seleman na kuongeza:
“Umechelewa kidogo tu ungepata picha zao yeye na mke huyo wa mtu
wakipiga mbizi uchi wa mnyama wakitokea gesti, sijui jana usiku walilewa
sana mpaka wamechelewa kuamka na kukutwa na mafuriko, muda huu wa saa
nne asubuhi!”
Aidha, juzi Alhamisi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ujenzi,
John Magufuli walifika eneo hilo la tukio na kujionea hali halisi.
Akizungumza na wananachi wa Kijiji cha Magole, Pinda aliwaambia
serikali imetoa chakula kwa waathirika wa tukio hilo na kuwataka wanachi
kuwa wavumilivu katika kipindi hicho kigumu walichopitia.