Like Us On Facebook

DIAMOND AWAPAGAWISHA WAKAZI WA LINDI KUFUNGA MWAKA 2013


 
Katika heka heka za kuaga mwaka 2013 usiku wa kuamkia leo mji wa Lindi ulitikisika baada ya mashabiki kujitokeza kushuhudia onyesho la Msanii nyota wa Muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alipokuwa akitoa burudan kabambe katika Tamasha la kudumisha Amani na Maendeleo lililodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Mtama,Mhe Bernard Membe na kufanyika katika Uwanja wa Ilulu Manispaa ya Lindi na kutoa burudani ya nguvu ambayo ilizikonga nyoyo za mashabiki waliodhuria
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’akiwapagawisha mashabikiw wake walikuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Ilulu,Mkoani Lindi.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’sambamba na madansa wake,wakitoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wao.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambae pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe akipokea salamu toka kwa Diamond alipokuwa akitoa salam za mwaka mpya kwa wana Lindi. 
>>Abdulaziz -Lindi
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari