Zamaradi Mketema.“Nilibadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu, Zamaradi akanifuatilia, juzijuzi nimerudi kundini (kwenye Ukristo) kwa kusikiliza maneno ya wazazi wangu, akanifuatilia tena.
“Huko
nyuma kupitia kipindi chake alikubali nidhalilishwe na waigizaji
wenzangu kwa faida yake (hakutaka kufafanua), iliniuma sana. Leo (hivi
karibuni) kaniweka hewani (kwenye redio) bila ya ridhaa yangu. Naomba
niseme kuwa naanza kugundua azma yake kwangu ni nini, aniache na maisha
yangu,” alilalama Wolper.Baada ya Wolper kulalamika sana, lilimtafuta Zamaradi kwa njia ya simu ya kiganjani ambapo alisema yeye anawajibika kwa kazi yake hakuna ishu ya kumfuatilia mtu.
“Mimi simfuatilii maisha yake, ni kazi tu. Kama mwandishi wa habari nikipata habari ya mtu natakiwa kubalansi (uwiano) naye,” alisema Zamaradi.

