
Ile kesi ya kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni Meneja wa Hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe Beach, Dar, Godlucky Kayombo iliyokuwa ikimkabili Wema Isaac Sepetu imetolewa hukumu yake kama ilivyokuwa ile ya shosti’ake, Kajala Masanja.
Habari kutoka kwa chanzo makini  kilieleza kuwa Wema 
alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu au faini ya shilingi laki moja kwa 
maana ya elfu hamsini kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia ya kutenda
 makosa hayo mawili ya kupiga na kutukana.
WEMA AOMBA IHARAKISHWE
Habari za ndani kutoka 
kwa mtu wa karibu wa Wema au Madam zilieleza kuwa hukumu ya kesi hiyo 
ilikuwa iahirishwe lakini staa huyo akaomba itolewe kwa kuwa alitaka 
kusafiri.
Ilisemekana kuwa mbali na kuwa na safari pia aliomba 
itolewe kwa sababu yupo ‘bize’ na maandalizi ya arobaini ya baba yake, 
Isaac Sepetu aliyeaga dunia hivi karibuni.
Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe, Dar ambako 
ndiko kesi hiyo ilipokuwa ikirindima tangu mwezi Agosti, mwaka huu.
ASUBIRIWA KUPELEKWA GEREZANI, ACHOMOA ‘MADOLARI’
Ilielezwa kuwa katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa takriban saa mbili, 
Wema alikuwa akisubiriwa nje tayari kupelekwa gerezani lakini kama 
kawaida yake fedha iliongea ambapo alizamisha mkono laini kwenye ule 
mkoba wake na kuchomoa ‘madolari’.
Chanzo kilidai kuwa zilihitajika 
fedha za Kibongo hivyo Wema alichambua mkoba wake na kutoa ‘wekundu’ 
kumi huku akirejesha zile dola za Kimarekani.
“Wema alifanya kama alivyomfanyia Kajala siku ile pale Kisutu. Kwa 
Wema ishu ya fedha siyo tatizo sana. Kuliko kumpotezea muda, Wema yupo 
tayari kutoa kiasi chochote cha fedha.
“Kwa Wema muda ni kitu cha 
muhimu zaidi kuliko hata hiyo fedha ndiyo maana alitoa tu hiyo faini 
mara moja,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupokea maelezo hayo, GPL  ilimsaka Wema ili kupata 
mzani wa habari hiyo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Hata hivyo, alipotafutwa meneja wake, Martin Kadinda na kuulizwa juu ya suala hilo alifunguka:
“Ile kesi iliisha tangu Ijumaa iliyopita, watu hawakujua tu. Wema 
alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu au faini ya shilingi laki moja.
“Alichokifanya Wema alilipa faini hiyo na sasa yupo freshi na mishe 
zinaendelea. Unajua haruhusiwi kufanya mahojiano hadi amalize arobaini 
ya baba yake.”
Chanzo kilisema kuwa kabla ya hukumu hiyo, Wema 
alikuwa katika hali kama ile iliyomkuta Kajala wakati wa hukumu yake 
miezi kadhaa iliyopita kwani alikuwa akilia, kujuta na kumuomba Mola 
amuepushe na balaa hilo lililosababishwa na kuwa ‘tilalila’.
Hata hivyo, hukumu hiyo iliwashangaza watu kwani iliendeshwa kwa muda
 mrefu na kwa mbwembwe nyingi lakini hukumu yake ikawa ya kawaida 
tofauti na matarajio ya wengi.
KAJALA NAYE KICHEKO TENA
Wakati Wema akikenua, 
wiki hii Kajala naye ilikuwa chereko chereko baada ya  Mahakama ya Rufaa
 Kanda ya Dar kuridhika na hukumu yake iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu
 Mkazi Kisutu mapema mwaka huu kufuatia rufaa iliyokatwa na mume wa staa
 huyo Faraji Chambo.
Katika kesi ya awali, Kajala alihukumiwa kifungo cha miaka mitano au 
faini ya Sh. milioni 13 baada ya kupatikana na hatia ya kushirikiana na 
mumewe kwenye msala wa kutakatisha fedha haramu wakati mwanaume huyo 
akifanya kazi Benki ya NBC, Dar.
Hata hivyo, Wema alimlipia faini hiyo kama alivyofanya kwenye kesi yake.
Katika hukumu ya rufaa hiyo, majaji walijiridhisha kwamba kesi hiyo 
iliendeshwa ipasavyo na Kajala alitimiza taratibu za kuwa huru kwa 
kulipa faini lakini mumewe aliyehukumiwa miaka saba alishindwa kulipa 
faini ya Sh. milioni 213.
MAOMBI YAO YASIKIKA
Wema na Kajala wamekuwa 
kwenye maombi ya kufunga wakisali na kufanya dua ili kuwaepusha na 
kifungo hivyo kwa sasa wote ni vicheko.
-GPL
-GPL

