Ripoti hiyo inabainisha kuwa Watanzania hao ambao
wanaishi mijini na vijijini, wanapata Sh26,000 kwa mwezi, ambayo ni sawa
na Sh866 kwa siku.
Akizindua Toleo la Nne la Taarifa ya Hali ya
Uchumi nchini jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa WB, Philippe
Dongier alisema hali hiyo inatisha.
Dongier alisema mpango huo ulifanikiwa kwa kiasi
kikubwa nchi za Brazil na Mexico na kwamba, nchini umetekelezwa wilaya
za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(Tasaf).
Mtaalamu wa Uchumi wa Benki ya Dunia kwa nchi za
Tanzania, Burundi na Uganda, Jacques Morisset alisema asilimia 18.7 ya
wananchi wanaoishi mijini ni maskini, huku vijijini wakichukua asilimia
71.2.
Aliongeza kuwa asilimia moja ya wakazi wa Dar es Salaam, ni maskini wa kupindukia.
Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu Kitengo cha Kuratibu
Utendaji Ofisi ya Rais (PDB), Peniel Lyimo alisema siyo vyema kwa watu
kujadili kama Tanzania inaweza kuondoa umaskini uliokithiri au la,
badala yake waamini kwamba hali hiyo itakwisha nchini.
“Kwa namna ambavyo Serikali inatoa mchango mkubwa
kwenye kilimo, hasa kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
umaskini uliopindukia utakwisha,” alisema Lyimo.
Naye Meneja wa Sera za Uchumi wa WB kwa nchi za
Maziwa Makuu, Albert Zeufack alisema nchi nyingi zimeingia katika
umaskini kutokana na tabia ya Serikali zao kupenda kukopa fedha nyingi
hasa wakati wa uchaguzi mkuu kwenye nchi zao