TIMU ya Kilimanjaro Stars imefanikiwa kusonga mbele
hatua ya Nusu Fainali baada ya kuwatoa Mabingwa watetezi wa Kombe hilo
Uganda kwa ushindi wa changamoto ya penalti 3-2 katika michuano ya kombe
la Chalenji inayoendelea jijini Nairobi, shujaa akiwa kipa Ivo Mapunda .
Katika
mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Manispaa ya mji wa Mombasa,
Uganda ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza likifungwa na
Daniel Sserunkuma katika dakika ya 16 akimalizia krosi ya Khamis Kiiza,
bao ambalo halikudumu sana kabla ya Mrisho Ngassa kuisawazishia Stars
kwa shuti kali nje ya 18.
Baada ya
bao hilo Stars walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la pili likifungwa
na Ngassa tena kwa mpira wa adhabu uliojaa wavuni katika dakika ya 39,
matokeo ambayo yalidumu mpaka mwisho wa kipindi hicho cha kwanza.
Kipindi
cha pili Stars inayofundishwa na kocha Kim Poulsen, raia wa Denmark,
ilipata pigo katikati ya kipindi hicho baada ya kiungo wake Salum
Abubakar 'Sure Boy' kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kucheza rafu,
ambapo nafasi hiyo iliwapa nguvu Uganda kupata bao la kusawazisha
kupitia Martin Mpuga matokeo ambayo yalibaki hivyo mpaka mwisho wa
mchezo na kuzipeleka mpaka kwenye matuta.
Katika mikwaju ya penalti Ivo alikuwa shujaa baada ya kucheza penalti mbili za Waganda ya beki Khalis Alucho na ile ya mwisho iliyopigwa na Sserunkuma ambayo ndiyo iliyoivusha stars.
Ifuatayo ni orodha ya waliopiga penalti katika mchezo huo.
Katika mikwaju ya penalti Ivo alikuwa shujaa baada ya kucheza penalti mbili za Waganda ya beki Khalis Alucho na ile ya mwisho iliyopigwa na Sserunkuma ambayo ndiyo iliyoivusha stars.
Ifuatayo ni orodha ya waliopiga penalti katika mchezo huo.
Kilimanjaro Stars Uganda
Erasto Nyoni (kakosa) Godfrey Walusimbi (kakosa)
Mbwana Samatta (kakosa) Emanuel Okwi (kapata)
Amri Kiemba (kapata) Khalis Alucho (kakosa)
Athuman Idd (kapata) Hamis Kiiza (kapata)
Kelvin Yondani (kapata) Sserunkuma (kakosa)