KATIKA
hali inayoonesha kuna kitu kikubwa kinakuja mbeleni, msanii wa filamu,
Chuchu Hans amejichora ‘tatuu’ inayosomeka kwa jina la Ray huku
anayedaiwa kuwa mpenzi wake, Vincent Kigosi ‘Ray’ naye akiwa amejichora
tatuu inayosomeka kwa jina la Chuchu.
Ray na Chuchu.
Picha
ambazo gazeti hili limezinasa zinawaonesha wawili hao wakipigia ‘promo’
uhusiano wao huku wadau wengi wakiyafananisha mapenzi yao na ya njiwa.
Ili
kujua undani juu ya jambo hilo, mwandishi wetu aliwatafuta wasanii hao
ambapo Chuchu alionekana kukerwa na swali hilo na kujibu kwa ufupi kuwa
hataki kusumbuliwa.
“Hivi hamchoki kufuatilia maisha ya watu jamani? Naomba mniache,” alisema Chuchu Hans. Kwa upande wa Ray, simu yake ya mkononi iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.