Like Us On Facebook

MWANAMITINDO NA VIDEO QEEN "JACKY CLIFF" AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI CHINA...SOMA ZAIDI HAPA

Nchi ya Tanzania imeingia tena kwenye headline kuhusiana na suala la Madawa ya kulevya baada ya kukamatwa tena kwa Mtanzania mwingine akisafirisha Madawa hayo toka Thailand kuelekea Macao nchini China jumanne iliyopita.
Mtanzania huyo ni msichana ana jumla ya umri wa miaka 28 aitwae  Jackie Clief alikamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya Heroin huko Macao nchini China
a3853fb3862d450baca5a4282c0c0d81
Dawa hizo zimekutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na wana usalama kisha kufanyiwa X-ray ambapo baada ya kufanyiwa X-ray alikutwa na jumla ya vidonge 66 vikiwa na thamani ya dola za kimarekani 137,72.
fe5c726676e94e5fadbe9356a9ec599f
Msichana huyu aliliambia Jeshi la Polisi nchini China kwamba alikua akisafiri kuelekea Guangzhou ambao ni mji ulio chini ya jimbo la Guangdong huko China,Inasemekana Msichana huyu amewahi kushiriki video mbalimbali ikiwa ni pamoja na video ya Nataka kulewa ya Diamond.
Hii ni picha imepigwa akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Macao.
0f5d40554df94bcb9c99d45b4ef29b6a
     
Jack Cliff mwenyewe ndio huyu hapa

Jackie Cliff ambaye ni video queen wa Bongo anadaiwa kukamatwa na dawa za kulevya  nchini China. Star mmoja nchini aliyekataa kutajwa jina lake aliutonya mtandao wa  swahiliworldplanet  bila kufafanua zaidi kwa kusema kuwa Jackie amekamatwa na madawa ya kulevya China:
 
 "Jackie Cliff amekamatwa na unga China". alisema star huyo huku akitutumia na picha za mwanamke aliyefungwa kitambaa usoni baada ya kukamatwa na dawa hizo na mwanamke huyo anadaiwa ni Jackie Cliff. Angalia picha hizo hapo chini..........  
Hata hivyo baadhi ya mitandao jana  iliweka habari za mwanamke mmoja wa kitanzania kukamatwa na dawa za kulevya huko china lakini bado habari hizo hazikubainisha mwanamke huyo ni nani na usiku huu ndiyo ikasemekana ni Jackie Cliff. Habari hiyo inasomek  kama  ifuatavyo:

 
"Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

 
"Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.

 
"Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013."


TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari