Akisimulia mkasa mzima, mtoa habari hii
aliyetajwa kuwa dada wa marehemu anayejulikana kwa jina la Khadija,
alisema siku ya tukio kaka yake aliamka asubuhi na kumuaga kuwa
anakwenda bondeni kwa mkewe (Farida) kwa kuwa walikuwa nyumba tofauti.
Aliongeza kuwa, muda mfupi baada ya kaka
yake kuondoka nyumbani hapo, wifi yake (Farida) alifika nyumbani hapo
na kumwambia kuwa kaka yake ameumia sana aende akamuone.
“Mimi nilimshauri ampeleke hospitali tu
nikidhani ameumia kidogo, kwa sababu wamekuwa na kawaida ya kupigana
mara kwa mara na tulishawaonya. Wifi aliondoka na mimi nikaendelea na
shughuli zangu.
“Muda mfupi, uliingia ujumbe kwenye simu
yangu ya mkononi ukisomeka kuwa kaka yangu alikuwa amefariki dunia
huku ujumbe huo ukinionya kutolia ili nisimshitue mama,” alisema
Khadija.
Dada mwingine wa marehemu aliyejulikana
kwa jila la Christina, alisema yeye aliwahi kufika nyumbani kwa Farida
na kumkuta kaka yake akiwa amelala chali huku damu zikimvuja, muda
mfupi polisi waliwasili na kufanya taratibu zote muhimu.
Marehemu Amoni alizikwa siku chache
baada ya kufariki dunia kwenye makaburi ya Mburahati City jijini Dar
huku Farida akiwa mikononi mwa polisi kwa upelelezi zaidi.
vitukovyamtaa BLOG inatoa pole familia ya marehemu na linamuomba Mwenyezi Mungu ailaze pema roho ya marehemu Amosi-Amin.
-Gpl