SAKATA
la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Chadema),
kutuhumiwa kutumia vibaya madaraka yake, limeweka ndoa za wabunge
shakani.
Mbowe
juzi alituhumiwa na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM),
kubadilisha ziara ya Mbunge wa Viti Maalum, Joyce Mukya (Chadema),
aliyotumwa na Bunge nje ya nchi huku akiwa amechukua posho, asiende
alikotumwa badala yake aende Dubai katika Falme za Kiarabu na kurejea
nchini.
Wakimtetea
Mbowe, baadhi ya wabunge wa Chadema walifikia hatua kusema huo ni
uhusiano binafsi na kuongeza kuwa kama na wao wakianza kutaja, kila
mbunge ana uhusiano wa kifuska bungeni.
“Asubuhi
niliongea mambo ambayo niliwakwaza watu wenye familia zao, si wote
niliowakusudia kuwa ni mafuksa, wapo wachache naomba kuifuta kauli
yangu,” alisema Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Msabaha (Chadema),
alipogundua kosa alilofanya kuwatuhumu wabunge wote na vitendo hivyo
vichafu.
Baada
ya kufuta kauli huku akisisitiza bado baadhi ya wabunge wana tabia
hiyo, Mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah (CCM), alimpongeza Msabaha
kwa kitendo chake cha kiungwana na kuamua kuomba radhi na kufuta kauli
yake kwani tayari ilishahatarisha ndoa za wabunge wengi ndani ya Bunge
hilo.
“Nampongeza
Msabaha huu ndio uungwana naomba jambo hili liishe umewaokoa akinababa
wengi na akinamama ambao leo (jana) kutwa wameshinda wakipigiwa simu na
wenza wao wakiwahoji wewe wa kwako ni nani,” alisema.
Kabla
ya kauli hiyo, Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari (Chadema),
alitaka wabunge waache kuzungumzia masuala binafsi ya wabunge ndani ya
Bunge hilo, kwa kuwa endapo wabunge wote wakiamua kuzungumzia masuala
binafsi ya wabunge hao, Bunge hilo halitokalika.
“Kuna
mambo mengi yanafanyika huko nje tukiyaleta humu ndani hapatakalika,
wapo watu wanahusishwa mambo chungu nzima ya uvunjifu wa maadili, wapo
hapa wanahusishwa kuwa wana uhusiano na watoto wadogo, uongo, Bunge
tunaliacha kama sehemu ya mipasho tuache haya jamani,” alisema.
“Mimi
ni mtoto mdogo, lakini nasema Bunge ni sehemu ya kujadili masuala si
sehemu kujadili watu au maisha ya mtu binafsi, anakula nini au anafanya,
ni sehemu ya kujali maslahi ya watu,” alisisitiza.
--Habari Leo