Like Us On Facebook

LUSEKELO MZEE WA UPAKO AFUNGUKA BAADA YA KUPOKEA KIPIGO CHA MBWA MWIZI KUTOKANA NA WIZI WA PESA.

                        Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’.
 MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi jijini Dar es Salaam (GRC), Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ amekiri kuwa aliwahi kukamatwa kwa wizi wa pesa.
Mtumishi huyo wa Mungu ambaye hujiita Super Charge, alisema aliwahi kujikuta katika wakati mgumu baada ya kupokea kichapo cha kufa mtu kutoka kwa baba yake mzazi Mzee Anthony (sasa marehemu) baada ya kudakwa na wizi wa shilingi 900 akiwa nyumbani kwao Mbeya.
Tukio hilo lilimtokea akiwa kijana ambapo kisa hicho kilimsukuma kumrudia Bwana na kuamua kumshinda shetani
Akizungumza na Risasi Jumamosi hivi karibuni kanisani kwake Ubungo- Kibangu, Dar, Mzee wa Upako alisema hawezi kuisahau siku hiyo ambayo shetani aliamua kukunjua kucha zake kumwelekea yeye.
“Niliwahi kuiba shilingi 900, miaka ya zamani kidogo (hakutaja) tukio hilo lilinikumba lakini baba yangu alinipa kichapo cha kufa mtu hali ambayo ilinipelekea kuamua kumrudia Mungu aliye hai.
“Siku hiyo nilikuwa katika mihangaiko ya maisha lakini nilijua fedha hizo zingenisaidia kwa kipindi hicho, siwezi kusahau tukio hili maana baba yangu alinipiga sana, ilikuwa fedheha kwangu,” alisema Mzee wa Upako
Akizungumzia mchezo mzima ulivyokuwa, Mzee wa Upako alisema siku ya tukio, akiwa nyumbani kwao na ndugu zake, ghafla alikuta pesa ziko mezani kwenye chumba cha baba yake, aliamua kuzikwapua, lakini siku iliyofuata alitokea baba yake na kumshushia kichapo cha viboko ambavyo idadi yake haikumbuki.
“Hakika zilikuwa ni siku za majaribu kwangu, kukamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa pesa lilikuwa ni jambo ambalo sijawahi kulifanya achilia mbali kuliwaza kabisa, lakini siku hiyo sijui ilitokea nini nikajikuta nimenasa mtego huo mbaya na mchafu dhidi yangu,” alisema.
Licha ya kukaa kwa miaka kadhaa, njia sahihi ilikuwa ni kumrudia Muumba wangu. Jambo hilo halikumfurahisha marehemu baba yangu, alinimsamehe na kumuacha aendelee kumtumikia Mungu katika ngazi ya uchungaji.
-RISASI
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari