Like Us On Facebook

LADY JAYDEE AUGUA GHAFLA....ALAZWA HOSPITALI YA PRIMIER.

Mwanamuziki mwenye jina kubwa katika Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ hivi karibuni aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake Kimara-Temboni, Dar na kukimbizwa katika Hospitali ya Primier Care iliyopo  karibu na nyumbani kwake.

Akizungumza na paparazi wetu, ‘hazibandi’ wa staa huyo ambaye pia ni meneja wake, Gadna Habash ‘Kapteini’ alisema kuwa ‘waifu’ wake huyo alipata maambukizi katika koo lake hivyo akatumia dawa ambazo hazikustahili.




Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ akichezea simuHospitali ya Primier Care.
Gadna alifunguka kuwa   baada ya kutumia dawa hizo zilimletea homa kali ndipo walipomkimbiza katika hospitali hiyo na kugundua kuwa alitumia dawa ambazo hazikustahili kwa tiba ya koo hivyo walimlaza na kumuanzishia dozi nyingine.

“Mwanzo hata sisi tuliogopa sana kwa sababu alikuwa na homa kali   lakini  tulipomfikisha hospitalini waligundua kuwa alitumia dawa ambazo siyo tiba ya tatizo lake ambazo ndizo zilimdhuru, lakini hivi sasa yuko sawa na anaendelea na shughuli zake,” alisema Kapteini ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Maskani cha Radio Times FM.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari