Like Us On Facebook

KIPIGO CHACHOROPOA MIMBA YA AUNTY LULU

ILE mimba ya miezi mitano aliyokuwa nayo staa wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ imechoropoka kufuatia kipigo alichopewa na mpenzi wake.
Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Sosi wa karibu na mwigizaji huyo, amenyetisha habari kuwa, mwanaume huyo (jina kapuni) aliyedaiwa kuwa ndiye mwenye ujauzito huo ambaye maskani yake ni Kinondoni, jijini Dar, alimshushia kipigo Aunty Lulu kwa sababu ya kumuonea wivu kwani amekuwa akimzuia hata kuongea na simu.
Sosi huyo alizidi kutiririka na sentensi kuwa, kutokana na kipigo hicho, Aunty Lulu aliumia na kuanza kuvuja damu kisha akakimbizwa hospitali kwa Dokta Mvungi (Kinondoni) ambapo aliambiwa mimba imeharibika na kulazimika kusafishwa kizazi.
“Vikao vya kumsema mwanaume huyo kwa kosa alilofanya vilifanyika nyumbani kwao Jumapili ambapo aliahidi kutorudia tena na kuomba radhi huku akiahidi kumfanyia makubwa Lulu,” alisema sosi huyo makini.
Baada ya paparazi wetu kuzinyaka habari hizo, alimwendea hewani Aunty Lulu, alijibu kwa unyonge na kusema ndoto zake za kuwa na mtoto zimeyeyuka kufuatia kipigo hicho.
“Sina la kusema zaidi, ndoto za kuwa na mtoto zimeyeyuka mwanaume huyu amezidi wivu lakini sina jinsi kwa sababu ndio baba mtoto na ameshaomba msamaha,” alisema Lulu.
-GPL
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari