Kiungo
wa Arsenal Jack Wilshere huenda akaingia matatani baada ya kuwaonyesha
mashabiki wa Man City ishara ya matusi kwa kidole chake sekunde chache
baada ya mchezo ambao Arsenal ilifungwa 6-3 kumalizika.
Wilshere
akiwa anaonekana kukerwa na kelele za mashabiki hao ambao walionekana
kuimba nyimbo za kumdhihaki aliwaonyesha kidole cha kati ishara ambayo
hutafsiriwa kama tusi sehemu mbalimbali duniani.
Kutokana
na kitendo hicho Wilshere yuko hatarini kukumbwa na rungu la chama cha
soka cha England FA ambao kwa vyovyote watalifanyia uchunguzi tukio hilo
kabla ya kulifanyia maamuzi.
Mara
nyingi wachezaji wanaofanya kosa kama hilo hukumbana na hatua za
kinidhamu ikiwemo kutozwa faini pamoja na kupewa adhabu ya kufungiwa
mechi kati ya mbili na tatu.
Hii
itakuwa mara ya pili kwa mchezaji huyo kuingia matatani baada ya
kupigwa picha akiwa anavuta sigara ndani ya klabu ya usiku huko London
wiki chache zilizopita .
Wachezaji kadhaa akiwamo David Beckham na Luis Suarez wamewahi kukumbana na adhabu tofauti baada ya kufanya kosa kama hilo.