Aunt Ezekiel.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni nyumbani kwake
Mwananyamala jijini Dar, msanii huyo ambaye alibadili dini kutoka
ukristo na kuwa muislam baada ya kuolewa na mumewe, Sunday Demonte
alisema anajisikia kurudi kwenye ukristo kwa madai ya kumtumikia Mungu
kikamilifu.Akionesha msisitizo katika hilo, Aunt alisema moyo wake umekuwa ukitamani kusikiliza mafundisho na mahubiri ya kikristo pamoja na kusikiliza nyimbo mbalimbali za injili.
“Natamani sana kuokoka, mara nyingi nikisikia mahubiri au nyimbo za injili, moyo wangu hupata faraja kubwa sana,” alisema Aunt.
Wakizungumzia mawazo ya kuokoka ya msanii huyo, baadhi ya mashabiki wake walimshangaa huku wakionesha wasiwasi wake juu ya kusilimu na kudai huenda kubadili kwake dini ilikuwa danganya toto.
“Huyu si aseme tu uislam umemshinda? Kasilimu juzijuzi tu hapa na kudai ameanza kusali msikitini, leo anatuambia anatamani kuokoka, hawa mastaa wetu wanamchezea sana Mungu,” alisema Rahma wa Kinondoni jijini Dar.