Like Us On Facebook

AIBU:KINGWENDU AGEUKA TAPELI AKIMBILIA MSUMBUJI NA MKWANJA WA DIRECTOR

Mchekeshaji maarufu Kingwendu anatuhumiwa kumtapeli mtayarishaji wa filamu za kitanzania ‘Bongo Movies’ ambaye pia ni mshindi wa tuzo za ZIFF, Bondi.
Akiongea kupitia kipindi cha Filamonata cha 100.5 Times Fm, kinachoongozwa na Monalisa na mama yake ‘Natasha’, Bondi amesema kuwa alimlipa pesa mchekeshaji huyo ili aweze kuigiza kwenye filamu yake na kusaini mkataba, lakini alipotea na kuelekea Msumbiji huku simu yake ikiwa haipatikani.
“Nilimpa fedha ya advance akachikichia moja kwa moja kumbe ana shows zake anaenda kufanya huko Mozambique. Kwa hiyo imefika siku ya kufanya filamu ambapo nilikuwa nashuti mimi, Kingwendu hayupo na siku sita amezima simu haipatikani.” Amesema Bondi.
Lakini kukosekana kwa Kingwendu kulimpa shavu mchekeshaji mwenzake Bambo, “Nikaamua nifanye option B, Option B niliyofanya nikamtafuta Bambo nikaongea naye, nikaelewana naye vizuri na tukafanya kazi.” Ameeleza producer Bondi.
Naye Kambarage wa kampuni ya usambazaji wa filamu ya Steps Entertainment, amesema kwa kuwa Kingwendu amevunja mkataba na kumuingizia Bondi gharama za ziada, kampuni ya Steps imepanga kuongea na Kingwendu na endapo ataenda kinyume watamfungulia mashitaka ili iwe fundisho kwa wasanii wenye tabia kama yake.
Filamonata inakuwa hewani kila Jumapili kuanzia saa 5 kamili asubuhi hadi saa 7 mchana kupitia 100.5 Times Fm.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari