Baadhi ya Wataalamu wa kufichua watu wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina na uchawi maarufu KAMCHAPE wamejikuta wakiwa kwenye mikono ya dola baada ya kuendesha zoezi la kufichua uchawi katika nyumba kadhaa kwenye vijiji mbalimbali vya manispaa ya Tabora ambapo baadhi ya wananchi walililalamikia zoezi hilo kwa madai kwamba limekuwa likiwadharirisha baadhi ya watu pamoja na kujenga chuki ambazo huenda zikasababisha madhara makubwa katika jamii.
Hapa
ni baada ya kufikishwa kituo kikubwa cha Polisi mjini Tabora kwa amri
ya Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya ambapo aliwataka kuacha
mara moja zoezi hilo la kufichua wachawi.