Like Us On Facebook

WABONGO WATENGENEZA PICHA FEKI ZIKIMWONYESHA MHESHIMIWA GODBLESS LEMA AKIFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE...!


Mbunge wa Arusha mjini Godbles amekanusha  na kukemea vikali baadhi ya watu wanaomdhalilisha kwenye mitandao ya kijamii kwa kutengeneza na kusambaza picha chafu ambazo zinaonesha udhalilishaji mkubwa kwa mbunge na hata kwa mtu wa kawaida.
 
Akizungumza  na vyombo vya habari ofisini kwake jijini Arusha mbunge Lema amesema picha hizo za aibu zimetengezwa na kusambazwa na mtu ama watu wenye lengo la kumdhalilisha na tayari amekwishaanza hatua ya kuchukua hatua za  kufikisha suala hilo kwenye uongozi wa bunge akiwemo Spika Anne Makinda, naibu spika Job Ndugai pamoja na katibu wa bunge.
 
Amesema ameamua kutoa taarifa hiyo kwenye vyombo vya habari kwa sababu vitu vikishawekwa kwenye mitandao ya kijamii siyo siri tena hivyo anategemea bunge litaona wajibu na ni jinsi gani heshima ya mbunge imeshushwa na kudhalilisha kwa maksudi bila kujali utu na heshima ya mbunge.
 
MSIKILIZE HAPA CHINI LEMA AKIZUNGUMZIA ALIVYODHALILISHWA 
 Mbunge Lema amefafanua kwamba picha hizo hazijatengenezwa na mbunge wa Iramba Muhigulu Nchemba kama baadhi ya watu walivyomfikishia taarifa kwani akiwa bungeni mjini Dodoma alizungumza na Nchemba na kubaini kwamba alikuwa hajaziona picha hizo hivyo hakuwa anajua lolote juu ya suala hilo. 


 MSIKILIZE LEMA HAPA AKISEMA NCHEMBA HAKUHUSIKA KWENYE PICHA  
 MSIKILIZE HAPA CHINI MKE WA LEMA 
 
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari