Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya ndani Mh Dk
Emanueli Nchimbi wakati wa uzinduzi wa dawati la jinsia pamoja na
mpango kazi wa miaka mitatu unaaonyesha majukumu ya jeshi la polisi
katika kuimaraisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Naye mkuu wa jeshi la polosi nchini IGP Saidi Mwema
amesema tangu kuanza kufanyiwa majaribio mpango huo umeonyesha
mafanikio makubwa na hivyo ameitaka jamii kujitokeza na kutumia dawati
hilo.
Akizungumza katika hadhara hiyo mratibu mkazi wa
umoja wa mataifa Bw Aliberic Kacou amewataka viongozi kuhakikisha kuwa
wanatumia nafasi zao pamoja na sheria zilizopo kuhakisha kuwa
wanawadhibiti wale wote ambao kila mara wamekuwa wakifanya vitendo vya
kikatili kwa makusudi.
-ITV
-ITV