ILIKUWA Novemba 28, mwaka 2011, Arsenal ilipoondoka imetota vibaya Uwanja wa Old Trafford ikitandikwa mabao 8-2, siku ambayo Wayne Rooney alifunga Hat-trick na Ashley Young akafunga mawili. Danny Welbeck pia alifunga.
Kwa
kiasi kikubwa Arsenal imekuwa ikinyanyaswa na Mashetani hao Wekundu,
wakiwa wameweza kushinda mechi moja tu ndani ya misimu 10 na wao
wakifungwa mechi 11.
Takwimu zote zinapatikana WhoScored.com, au fuatilia @WhoScored katika Twitter.
Man United 2-1 Arsenal, Ligi Kuu Novemba 3, 2012
Van
Persie alihitaji dakika tu kuwakumbusha mashabiki wa Arsenal kipi
watakosa kwa kuuzwa kwake kwa Pauni Milioni 24 kwenda Old Trafford,
akifunga bao la kwanza kwa guu la kulia. Patrice Evra akaifungia la pili
United baada ya mapumziko na Santi Cazorla akaipatia bao la kufutia
machozi Arsenal. Kipigo hicho kiliwaacha Arsenal na pointi 15 baada ya
mechi 10, mwanzo mbaya zaidi katika historia yao kwenye Ligi Kuu ya
England chini ya Wenger.
Man United 8-2 Arsenal, Ligi Kuu Novemba 28, 2011
Kipigo
cha 'mbwa mwizi' kilichotoka na Rooney kufunga hat-trick United ikijibu
kipigo cha Manchester City cha 5-1 msimu huo. Ikiwa imeathiriwa zaidi
na majeruhi na wachezaji kuwa nje wakitumikia adhabu, Arsenal ilikuwa
dhoofu haswa. Hakika ilikuwa moja ya siku mbaya sana kwa Wenger kazini.
"Tulivunjika nguvu kipindi cha pili, ni maumivu makubwa,"alisema kocha
huyo wa Arsenal.
Matatu kiulaini: Rooney alifunga Hat-trick siku United ikiifumua Arsenal 8-2
Man United 2-0 Arsenal, KOmbe la FA, Machi 12, 2011
Pamoja na Arsenal kutawala sana mchezo, mwisho wa siku walichapwa. Wauwaji siku hiyo walikwa Fabio da Silva na Rooney.
Man United 1-0 Arsenal, Ligi Kuu, Desemba 13, 2010
Bao
tamu la kichwa la Ji Sung-Park lilitosha kuizamisha Arsenal mbele ya
United, siku ambayo mchezaji mpya wa Gunners Marouane Chamakh alipoteza
nafasi nzuri.
Man United 2-1 Arsenal, Ligi Kuu, Agosti 29, 2009
Siku
hiyo Arsenal walianza vizuri, Andrey Arshavin akitangulia kuwafungia
bao la kuongoza. Bao lilisawazishwa baada ya kipa Manuel Almunia
kumchezea rafu Rooney kwenye eneo la hatari aliyekwen kufunga kwa
penalti. Abou Diaby akajifunga mwenyewe dakika tano baadaye kuipa United
bao la ushindi. Wenger akapandishwa jukwaani baada ya kutupa chupa
dakika ya 95, kufuatia bao zuri la kusawazisha lililofungwa na Van
Persie kukataliwa akiambiwa aliotea.
Man United 0-0 Arsenal, Ligi Kuu Mei 16, 2009
Arsenal
ilikwenda Old Trafford kwa lengo la kuwabania United wasitwae taji
mapema, baada ya kuwa tayari wamebeba taji la Ligi ya Mabingwa mwezi
uliotangulia. Lakini pamoja na yote, United walipata ponti waliyoihitaji
kubeba taji la 11 la Ligi Kuu wakiwa wamebakiza mechi moja – pia
wakafikia rekodi ya Liverpool kutwaa mtajai 18 jumla ya ligi hiyo tangu
inaitwa Daraja la Kwanza.
Man United 1-0 Arsenal, Ligi ya Mabingwa, Aprili 29, 2009
Arsenal
walikuwa wenye bahati sana kufungwa bao moja siku ambayo United
walishindwa kutumia vizuri nafasi walizotengeneza kwa matunda ya kucheza
vizuri. Timu ya Ferguson ilipeleka sukrani zake kwa John O’Shea
kuwasogeza jirani na fainali ya Ligi ya Mabingwa. Arsenal ilitumai
kuzinduka katika mchezo wa marudiano nyumbani, lakini siku hiyo
hawakufanya kosa baada ya kukifumua kikosi cha Wenger mabao 3-1 na
kuifuata Barcelona katika fainali.
Man United 2-1 Arsenal, Ligi Kuu, Aprili 13, 2008
Arsenal
ilipata nafasi lakini ikashindwa kuitumia kuimaliza United, baada ya
Adebayor kuwafungia bao la kuongoza dakika mbili baada ya mapumziko
ingawa mkono ulihusika katika bao hilo hilo. United ilisawazisha kupitia
kwa Ronaldo kwa penalti baada ya William Gallas kuunawa mpira kwenye
eneo la hatari, kabla ya Owen Hargreaves kuifungia United bao la ushindi
kwa shuti la mpira wa adhabu umbali wa mita 25 na kuifanya ipae
kileleni kwa pointi sita zaidi.
.
Man United 4-0 Arsenal, Kombe la FA, Februari 16, 2008
Ferguson
aliamua kuwapumzisha Ronaldo na Ryan Giggs, lakini Rooney alitosha
kuwamaliza akifunga bao la kwanza wakati Darren Fletcher alifunga mawili
na Nani moja. Rooney alijitengenezea nafasi katika kikosi cha kocha wa
England wakati huo Fabio Capello, huku United ikitinga Robo Fainali,
ambako kwa bahati mbaya walitolewa na Portsmouth walioibuka mabingwa.
Man United 0-1 Arsenal, Ligi Kuu Septemba 17, 2006
Baada
ya kucheza mechi tatu bila kushinda tangu mwanzo mwa msimu, Arsenal
ilizinduka zikiwa zimebaki dakika tano mchezo kumalizia, Fabregas
alipompokonya mpira Cristiano Ronaldo kabla ya kumpasia Emmanuel
Adebayor ambaye alimtungua Tomasz Kuszczak. Pamoja na hayo mwisho wa
msimu, United iliibeba taji kutoka kwa Chelsea huku Arsenal ikiachwa kwa
ponti 21 nafasi ya nne.
Man United 2-0 Arsenal, Ligi Kuu, Aprili 9, 2006
Mabao
ya Rooney na Ji-Sung Park yalitosha kuimaliza Arsenal huku United
ikiweka rekodi ya kushinda mechi a tisa mfululizo katika ligi.
Man 1-0 Arsenal, Kombe la Ligi, Desemba 1, 2004
Manchester
United kwa mara nyingine waliitambia Arsenal iliyokuwa imesheheni
makinda waliosajiliwa na Wenger kama Robin van Persie wakati Ferguson
alikuwa ana wakali kama Eric-Djemba Djemba na Kleberson. Mchezaji
mwingine ambaye hakufika mbali, David Bellion, ndiye aliyefunga bao hilo
pekee sekunde ya 19.
Man United 2-0 Arsenal. Ligi Kuu Oktoba 24, 2004
Van Nistelrooy alitangulia
kufunga dakika ya 72 kwa penalti, na Rooney akafunga la pili dakika ya
90 kumaliza rekodi ya Arsenal kutofungwa ndania ya mechi 49.
Man United 0-0 Arsenal, Ligi Kuu Septemba 21, 2003
Mechi
kali ndani ya Old Trafford. Baada ya dakika 80 mechi ilichafuka baada
ya Ruud van Nistelrooy kuonyeshana ubabe na Patrick Vieira. Kisha katika
dakika za lala salama Van Nistelrooy alikosa penalti baada ya Martin
Keown kumchezea rafu Diego Forlan.
Hiloo: Martin Keown akimzomea Ruud van Nistelrooy baada ya Mholanzi huyo kukosa penalti