Mwanafunzi aliyekuwa akisoma
shule ya sekondari Sabasaba mjini Iringa akijiandaa kurudia
kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne kupitia kituo cha
Krelluu mjini Iringa Khamis Mkundo mkazi wa Mwangata C katika
manispaa ya Iringa amejiua kwa kujinyonga kwa kamba kwa kile
alichodai kuchoshwa na kufeli mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.
Katika barua yake ndefu
aliyoiandika kijana huyo amesema kuwa amefanya hivyo si kwa
kujipendea ila amechukizwa na hatua yake ya kufeli mara kwa mara
hivyo kuamua kujiua ili kuepuka aibu katika mtihani ujao ambao
anaamini angefeli.
Shemeji wa kijana huyo Aden Tagalile
ameueleza mtandao matukiodaima.com kuwa tukio hilo
limetokea mida ya saa 12 na saa 1 usiku wa leo baada ya
kuwepo kwa mazungumzo ya muda mrefu kwa kijana huyo kuonyesha
kuchukia hatua yake ya kuendelea kuristi mtihani wa kidato cha nne
bila mafanikio.
Kijana huyo alisema hajapenda kuona anaendelea kufeli na kuwa yupo tayari kwa lolote kukwepa aibu ambayo ipo mbele yake.
Hata hivyo kufuatia mazungumzo hayo, kijana huyo aliagana na ndugu zake akiwemo kaka yake anayeishi nae kwa
kila mmoja kuondoka nyumbani hapo kabla ya kijana huyo kukutwa
amejinyonga.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo
Sarehe Mgimwa amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuonyesha ujumbe
ambao kijana huyo ameuacha .
-Matukiodaima .com