Mama Mzazi wa Mwanafunzi anaedaiwa
kubakwa, Mary Mkombola akisimulia juu ya tukio la ubakaji lililompata
Mwanae na kusababisha ujauzito mbele ya waandishi wa habari Kulia ni Martha Danie (17) anayesoma shule ya City Sekondari kidato cha tatu aliyefanyiwa kitendo hicho.
Mwanae na kusababisha ujauzito mbele ya waandishi wa habari Kulia ni Martha Danie (17) anayesoma shule ya City Sekondari kidato cha tatu aliyefanyiwa kitendo hicho.
Mwanasheria Mfawidhi Mkazi wa kituo cha msaada wakisheria cha Tanzania Legal Aid Centre (TALAC), Godwin Ngongi akifafanua jambo kuhusu kitendo cha ubakaji alichofanyiwa Mwanafunzi wa kidato cha tatu Martha
Nabii Elisha Muliri anayetuhumiwa kwa ubakaji
NABII Elisha Muliri wa kanisa
la Ebeneza mjini hapa ameingia matatani baada ya kudaiwa kumbaka na kumtia
mimba mwanafunzi na kukatiza masomo yake huku kutishia kumuua.
Akisimulia tukio hilo mbele ya
waandishi wa habari mwanafunzi huyo Martha Daniel [17] kidato cha tatu katika
shule ya sekondari ya City ilyopo manispaa ya Dodoma alisema kabla ya kufanyiwa
kitendo hicho alikuwa anaangushwa na mapepo.
Martha alisema baada ya kuhangaika
kwa muda mrefu bila mafanikio walipata taarifa za ujio wa nabii huyo mjini humo
na wapofika ili kupata msaada wa kuombewa mapepo hayo yalilipuka na binti akaponywa
hata leo na kuahidiwa mbele ya kanisa kusaidiwa ada na Nabii huyo.
Binti huyo alisema baada ya kuponywa
akaendelea kwenda kusali kanisani hapo ambapo kutokana na kila mtu anayefika na
kufanyiwa maombi huacha mawasiliono kwenye vikaratasi, na Juni 8 mwaka huu
majira akapigiwa simu na Nabii huyo akipewa maelekezo ya kufika nyuma ya ukumbi
wa Paradise ambapo walikuwa wakifanyia ibada.
Anatanabaisha kuwa baada ya kuonana
Nabii alimwambia aingie kwenye Gari akaingia akifikili kuna heri akapewa soda
aina ya Fanta orange alipokunywa akapoteza fahamu na alipokuja kuzinduka
alijikuta akiwa nyumba za kulala wageni makole na Nabii akiwa amemlalia kama
alivyozali huku akiangalia mkanda wa Ngono.
‘’Wakati nataka kupiga kelele
alinitishia kwamba ataniua kama nitathubutu kumwambia mtu yoyote jambo hilo,
akanipiga kofi na kuniambia yeye hawezi kunilipia ada bure kwa sababu mimi siyo
ndugu yake lazima lazima alale na mimi mara 5 kwa hiyo bado mara 4 na
kunisisitiza asisikie popote kuwa alinifanyia hivyo’’, alisema Mwanafunzi huyo
Kwa upande wake Mama mzazi wa
mwanafunzi huyo Mary Mkombora alisema alimpeleka kuombewa kutokana na
kusubuliwa na mapepo tangu akiwa Darasa la sita na wakakubaliana na Nabii huyo
kumlipia ada kwa awamu hivyo akachukue 50,000 kila mwezi ili kukamilisha
400,000 inayotakiwa shule.
Nilimgundua yupo tofauti kuanzia
mwezi wa saba nilipomuuliza alisema yeyue haelewi siku moja nikamshuhudia
akitapika asubuhi ndipo nilipochapa na kumfukuza nikapigiwa simu na waliompokea
kua mtoto kapewa mimba hiyo na Nabii kwanini nimemfukuza ndipo nikachoka,
alipopimwa alikuwa na mimba.
Alisema Nabii huyo ambaye alikuwa
Mume wa mwimbaji Marufu wa Nyimbo za Injili marehemu Anjera Chibalonza kwa sasa
hajulikani alipo japo mara kadha wasaidizi wa kanisa hilo ambalo limebadilishwa
jina kutoka Shakinah Pentecostal Church na kuitwa Ebeneza wamekuwa akitaka
Suruhu.
‘’sasa hivi mimi na mtoto
wangu tumekuwa tukiishi mashakani baada ya Msaidizi wake Nabii Monica
nimpe Martha akamtoe mimba kwa ataaramu anaowajua wao, siku ambayo alichukua
kadi yenye namba za simu na kufuta meseji zote mwanangu alizokuwa akiandikiwa
na Nabii,’’
Nabii huyo kwa sasa hajulikani alipo
na hata alipotafutwa kwa simu yake ka mkono 0756
409118 ilikuwa amezimwa na msaidizi wake Nabii Monica Nyambura raia
wa nchini Kenya anakotoea Elisha Muliri alisema yeye hawezi kuongelea jambo
hilo kwakua yeye ni mgeni ameachiwa kanisa hilo baada ya mwenyeji wake kuwa
safarini hivya asubiliwe hatachelewa.
Tukio hilo limefikishwa katika kituo
cha sharia cha Tanzania Legal Centre [TALAC] na mwanasheria mfawidhi mkazi
Dodoma Godwin Ngongi tayali ameshamuandikia mkuu wa kituo cha polisi kati barua
ya kuwataka kumkamata mtuhumiwa huyo ili afikishwe kwenye vyombo vya sharia na
pia kuepusha mwanfunzi huyo na hatari nyingine.
Jeshi hilo limekiri kuwa na taarifa
ya tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi.