Mwanaume wa China ameshinda kesi ya kulipwa $120 000 ( tsh.192, 840,000/=) baada ya kumpa taraka mke wake kwa kumzalia watoto wabaya.
Awali, mwanaume huyo aitwaye Jian Feng, alikuwa akimtuhumu mke wake
kuwa anatoka nje ya ndoa kwakuwa haikuwa ikimuingia akilini kuzaa watoto
wasiovutia kama wao..
Baada ya DNA kuweka bayana kuwa kweli watoto ni wa kwake, mke wa Feng
aliamua kuitoa siri nyingine ndogo.
Kabla ya wanandoa hao kukutana, mke wa Feng alikuwa amefanyiwa upasuaji wa urembo (cosmetic surgery) uliogharimu $100,000 nchini Korea Kusini na ndio maana watoto waliozaliwa walikuwa tofauti na wazazi.

Feng alimshitaki mke wake kwa kuficha ukweli huo na kumfanya amuone
mrembo. Kutokana na maelezo hayo, jaji alimpa ushindi Feng na kumwamuru
mke wake amlipe fidia ya dola $120,000.
Akiongea na Irish Times, Feng alisema: “Nilimuoa mke wangu kwa
upendo, lakini mara baada ya kupata mtoto wa kwanza tulianza kuwa na
migogoro. Binti yetu alikuwa mbaya haswaa, hadi kufikia wakati akawa
ananitisha.”