Mtoto
huyo ambaye ameshonwa nyuzi sita na amelazwa katika chumba cha wagonjwa
mahututi katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, anadaiwa kufanyiwa ukatili
huo na mkazi wa Madizini, Ronginus Haule (50), akimtuhumu kuiba mapera
kwenye bustani yake.
Tukio hilo la kusikitisha na ambalo limekuwa gumzo mkoani hapa, limetokea juzi majira ya saa moja jioni.
Benson
ambaye ni mtoto wa pili wa mtangazaji wa Kituo cha Radio Maria Tanzania
mkoani Ruvuma, Jofrei Nilah, anaendelea kupata matibabu akiwa kwenye
chumba cha uangalizi maalumu (ICU ).
Akielezea
tukio zima, mama mzazi wa mtoto huyo, Rwosita Nyoni ambaye ni mke wa
Nilah, alisema kuwa mtoto wake hakuwepo nyumbani tangu majira ya saa
saba mchana, na alipomtafuta kwa ajili ya chakula cha mchana hakuweza
kumpata hadi ilipofika majira ya saa moja jioni.
Alisema
wakati anatoka kanisani, alikuta mkusanyiko wa watu wakimshangaa mtoto
ambaye alikuwa hafahamiki wa nani ambaye alikuwa ameumizwa vibaya na
kutapakaa damu mwili mzima huku akiwa amepoteza fahamu.
Alisema
wakati akijishauri kusogea eneo la tukio, alikuja jirani yake ambaye
alimtaja kwa jina la baba Said na kumshauri asogelee eneo la tukio
huenda akawa ni mtoto wake, na aliposogea aligundua kuwa ni mwanae
Benson jambo ambalo lilimshitua sana.
Kwa
mujibu wa habari hizo, Nilah aliamua kwenda polisi ambako alipatiwa
fomu namba tatu na kisha alimpeleka mtoto huyo katika hospitali ya Mkoa
wa Ruvuma kwa matibabu ambako alipokelewa na kulazwa wodi namba tano.
Muuguzi
wa zamu katika wodi hiyo, Erenesta Kapinga, alisema hali ya mtoto huyo
ni mbaya na wamelazimika kumhamishia kwenye wodi ya wagonjwa mahututi
kwa uangalizi zaidi.
“Tunahisi
amehumizwa ndani kwa ndani na damu zitakuwa zimevujia kwenye ubongo, na
sehemu za tumbo nazo atakuwa ameumizwa kwa sababu akikojoa anatoa damu,
hivyo kwa sasa tunasubiri majibu ya X-Ray ili tubaini ameumia eneo
gani,” alisema muuguzi huyo.
Mmoja
wa wanaharakati wa kituo cha wasaidizi wa sheria wanawake na watoto
mkoani Ruvuma, Fatuma Misango, ameelezea kusikitishwa na tukio hilo
ambalo alisema kuwa ni la uuaji, kwani umri wa mtoto na adhabu aliyopewa
haviendani.
Hata
hivyo, mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa Ruvuma (HOMSO), Dkt.
Benedicto Ngaiza amethibitisha kumpokea mtoto ambaye amejeruhiwa vibaya
kwa kupigwa mapanga usoni, na kwamba kwa sasa anaendelea kupatiwa
matibabu akiwa chini ya uangalizi maalumu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma,