Balozi
Isaac Abraham Sepetu alizaliwa October 15, 1943, ni mzaliwa wa Tabora
ila alikulia Zanzibar na alikuwa ni mkaazi wa Zanzibar mpaka mauti
yanamfika
Marehemu
Balozi Isaac Abraham Sepetu alipata elimu yake ya msingi na sekondari
katika shule ya St.joseph’s kwa sasa inaitwa Tumekuja huko Zanzibar
mnamo mwaka 1952 hadi 1963, vilevile aliweza kujiunga na chuo kikuu huko
Berlin nchini Ujerumani mwaka 1964 hadi 1970 alisomea Shahada ya
Uchumi,
Marehemu alikuwa anauwezo wa kuongea lugha tatu (3) kwa ufasaha ambazo ni ;- kiswahili, kingereza na kijerumani.
KAZI
Alianza
kufanya kazi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 1971 hadi 1972
kama Mkuu wa Bizanje Msaidizi na pia alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nchi
Ikulu. Baada ya hapo mwaka 1972 hadi 1977 alikuwa Naibu Waziri Mambo ya
Nje katika serikali ya Muungano Zanzibar, mnamo mwaka 1977 hadi 1979
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu alikuwa Waziri wa Habari na
Utangazaji, Ilipofika mwaka 1979 hadi 1982 alikuwa Waziri wa Utalii na
Maliasili .
Marehemu
Balozi Sepetu mwaka 1982 hadi 1989 alipewa nafasi ya kuwa Balozi wa
Tanzania nchini Urusi, Moscow na mwaka 1989 hadi 1990 alikuwa Balozi wa
nchi ya Zaire, Kinshasa
Katika Serikali ya Mapinduzi
Mwaka
1990 hadi 2000 alikuwa Waziri wa Nchi, Mipango pia alikuwa Mshauri wa
Rais, Ushirikiano wa Kimataifa na pia alikuwa Katibu , Kamati ya
Pamoja(IPC) CCM/CUF, Zanzibar Mwaka 2001 hadi 2005 alikuwa mbunge wa
bunge la Afrika ya Mashariki
Uzoefu wa Kisiasa
Mwaka 1977 hadi 2005 alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi