Mbunge wa Arusha Mjini mheshimiwa Godbless Lema jana alizua gumzo kwa wapiga kura wake baada ya kuamua kuzigawa picha za kutengeneza zilizokuwa zikisambazwa katika mitandao ya Kijamii zikimuonyesha akilawitiwa.
Gumzo hilo la aina yake lilitokea jana katika mkutano wake uliofanyika katika viwanja vya Kilombero jijini Arusha.
Muda mfupi baada ya mkutano huo kuanza, Lema alimuita Mke wake
(Neema) na kumtaka azigawe picha hizo kwa wananchi ambazo alikuwa ameziprint kwa wingi..
Wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo walikataa kupewa picha hizo na
kusema kuwa hazina umuhimu wowote kwao na wakamtaka mbunge huyo azichome moto kwa kuwa wanajua ni za
kutengeneza .
Baada ya mabishano ya dakika kadhaa, Godbless Lema aliamuru kura zipigwe kati ya wanaosema wapewe na wanaotaka zichomwe moto .Waliosema picha zichomwe moto walishinda.
Baada ya mabishano ya dakika kadhaa, Godbless Lema aliamuru kura zipigwe kati ya wanaosema wapewe na wanaotaka zichomwe moto .Waliosema picha zichomwe moto walishinda.
Baada ya kura hizo, picha zilichomwa moto na Lema akawashukuru wapiga kura wake
kwa kuonyesha heshima kwake kwa kuzikataa picha hizo.