Jacqueline
Wolper ameamua kurudi katika imani yake ya awali ya Kikristo ikiwa ni
miezi michache tangu alipotangaza kubadili dini na kuwa Muislamu.
Wolper akiwa katika Kanisa la KKKT lililopo Kijitonyama wakati wa ibada.
Novemba 3, mwaka huu (Jumapili iliyopita) mwandishi wetu alimnasa
Wolper katika Kanisa la KKKT lililopo Kijitonyama jijini Dar, akisali
sambamba na waumini wa kanisa hilo.
Waumini wakiendelea na ibada ndani ya kanisa alimokutwa Wolper.
Bila ya kificho, Wolper ambaye alipokuwa Muislamu alikuwa akitumia
jina la Ilham alisimama na kujitambulisha kama muumini mpya wakati
mchungaji wa kanisa hilo alipowataka waumini wapya kufanya hivyo.
Wolper akiwa katika ibada kanisani hapo.
Wakati ibada hiyo ikiendelea, Wolper alionekana kuimba pambio kwa
hisia kali na ibada ilipoisha, alitoka kanisani huku mkononi mwake akiwa
ameshika Biblia.
Wolper (kulia) akiwa na muumini mwenzake nje ya kanisa.
Nje ya kanisa hilo, Wolper alionekana akiongea na wazee wa kanisa
pamoja na baadhi ya waumini ambapo wote walimkaribisha kwa furaha.
Jacqueline Wolper akiwa katika vazi la Kiislamu wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan mwaka jana.
Mwandishi wetu alimfuata Wolper na kumuuliza kilichomfanya arudi
kwenye dini yake ya awali, naye alisema kwamba amefanya hivyo kutokana
na msukumo wa wazazi wake ambao kwa muda mrefu walikuwa wakipinga
kitendo chake cha kuwa Muislamu.
“Nimeamua kuurudia Ukristo kwa kuwa wazazi wangu kwa muda mrefu
walikataa mimi kuwa Muislamu, kwa hiyo kuanzia sasa siyo Ilham tena,
niite Jacqueline kama zamani,” alisema Wolper.
Wolper akiwa ndani ya gari aina ya BMW X6 alilonunuliwa na Abdallah Mtoro ‘Dallas’ baada ya kubadili dini na kuwa muislamu.
Mwaka jana, Wolper alibadili dini na kuwa Muislamu kutokana na kuwa na uhusiano na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
Dallas akiwa nje ya nchi akamtaka Wolper kubadili dini ili akirudi
wafunge ndoa ya Kiislamu, Wolper alikubali na kufanya hivyo katika
Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar na kuchagua jina la
Ilham.
Gari aina ya BMW X6 alilonunuliwa Wolper na Dallas baada ya kuwa muislamu.
Dallas alirudi nchini lakini wawili hao hawakufunga ndoa bali penzi
lao likaingia doa na kumwagana, Wolper akaendelea na msimamo wa imani
yake hiyo mpya na mara kwa mara alikuwa akidai kwamba hataiacha dini
hiyo pamoja na kumwagana na Dallas.
---GPL