
Raia hao wa Uingereza, Kirstie Trup na Katie Gee, 
hivi sasa wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali za Chelsea na 
Westminster London na taarifa zinaeleza kuwa afya zao zimeimarika kwa 
kiwango cha kuridhisha hasa baada ya kufanyiwa upasuaji na kisha 
kuwekewa ngozi upya. 
Pamoja na madhara waliyokumbana nayo raia hao wamesema kuwa bado hawajakatishwa tamaa na tukio hilo na sasa wanapanga kurejea tena visiwani humo kuendelea na kile walichokiita ‘kazi za upendo’.
  
                
              Pamoja na madhara waliyokumbana nayo raia hao wamesema kuwa bado hawajakatishwa tamaa na tukio hilo na sasa wanapanga kurejea tena visiwani humo kuendelea na kile walichokiita ‘kazi za upendo’.
Katika waraka wake uliochapishwa na Gazeti na 
Daily Telegraph, Kirstie Trup amesema kuwa yeye na mwenzake wamepanga 
kurejea Zanzibar mwaka ujao na kwamba safari hii wataongeza kasi ya 
kushiriki kazi za kujitolea.
  
                
              
“Kwa sasa tuko imara na mwakani tumepanga kurejea 
tena visiwani Zanzibar kushiriki katika kazi za kujitolea,” alisema Trup
 ambaye ngozi yake imefanyiwa ukarabati wa kisayansi na kuwekewa ngozi 
upya katika eneo la mkono wa kulia na sehemu ya bega.
  
                
              
Akielezea zaidi kuhusiana na tukio hilo la 
kumwagiwa tindikali, Trup alisema kuwa anachokumbuka ni kuwa wakati 
akiwa na mwenzie wakielekea mgahawani ghafla walijitokeza watu wawaili 
na walipowakaribia walichomoa kopo kutoka kwenye mfuko na kumwaga kitu 
cha majimaji ambacho baadaye kilibainika kuwa ni tindikali.
  
                
              
“Mwili mzima uliwaka kama vile nimechomwa na moto.
 Maumivu yalikuwa makali sana yasiyoweza kuelezeka hasa katika eneo la 
bega langu la kulia. Nachokumbuka kingine ni kuwa tulipiga kelele kwa 
sauti sana hata kufanya wale waliokuwa kwenye hoteli iliyokuwa jirani na
 sisi kutahamaki,” alisema Trup.
  
                
              
Amesema kuwa baada ya tukio hilo alijitokeza 
mtalii ambaye aliwapa msaada kwa kuwamwagia maji sehemu walizojeruhiwa 
na baada ya hapo walijitosa baharini katika kile walichoeleza ni 
kujaribu kutuliza maumivu.
  
                
              
“Yule mtalii alituonyesha moyo wa ukarimu sana 
maana alituhudumia vizuri na baadaye tulichojoa nguo zetu na kujitupa 
baharini kwani maumivu yaliendelea kuongezeka na hali izidi kuwa mbaya 
maana hata rangi ya ngozi yangu ilianza kubadilika,” alisema.


 
 
 
 
 
