Mabasi yaendayo mikoani leo
asubuhi yamegoma kufanya safari zake kama ilivyo ratiba zake za kawaida,
kwa madai kwamba walikuwa kwenye mgomo. Mwandishi wetu John Chacha
alipofika katika Kituo kikuu cha mabasi Ubungo alikuta mabasi yote
yakiwa yamepakia abiria lakini hayakuwa yametoka kufuatia wamiliki wa
mabasi hayo kuwakataza madereva kuyatoa mabasi hayo kama ilivyo
kawaida.
Mabasi hayo yamegoma kufuatia mgomo wa malori uliosababishwa na ongezeko la tozo la asilimia 5 katika mizani.
Baadhi ya abiria wakiwa njia panda katika kituo cha mabasi Ubungo