Like Us On Facebook

"SITAKI KUZAA NA MWANAUME WA BONGO,LABDA KWA NDOA YA MKATABA..." AVANA

AVANA mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MSANII wa kike wa filamu Bongo anayetamba na filamu za Asili Swahiliwood Husna Chobis ‘Avana’ amedai kuwa hataki kuzaa na mwanaume wa Bongo kwa sababu wengi ni walaghai, na kwa sababu yeye ni maarufu anapata wakati mgumu kumjua ni mwanaume gani anaweza kuwa mkweli kwake, anaweza kuwa anamtamani kwa sababu ya jina lake tu.

husna athuman chobis 605

“Sitaki kuzaa na mwanaume asiyeeleweka wengi ni walaghai anakutumia tu kisha anakutelekeza sasa wana nini? Bora kwa nchi za wenzetu kuna kuwa na ndoa za mikataba unajua kabisa nitakuwa na mtu huyu kwa muda fulani nizae naye au tule raha tu mwazo mwisho,”anasema.
Avana ambaye anatamba na filamu ya Gawa iliyotengenezwa na Mussa Banzi anasema kuwa tayari alishawahi kuumwa na nyoka baada ya kuolewa na kusumbuliwa hadi kuachana na mumewe jambo ambalo hataki litokee katika maisha yake tena na hataki kuzaa na mwanaume wa Bongo labda kwa ndoa ya mkataba kama Ulaya.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari