Katibu mkuu kiongozi BALOZI OMBENI SEFUE amesema mfumo huo utaongeza uwazi zaidi Serikalini na uwajibikaji hali itakayowezesha wananchi kuwasiliana moja kwa moja na Serikali.
BALOZI SEFUE akikagua maendeleo ya uanzishwaji wa utaratibu huo wa kufanya kazi kwa njia ya mtandao kwa Wakala ya Serikali Mtandao Tanzania waliopewa dhamana hiyo amesema upo mpango wa kupeleka huduma za TEHAMA katika kila kijiji nchini ili kuharakisha maendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa wakala ya Serikali Mtandao Dk. JABIR BAKARI amesema wanafanya maandalizi ya kuhakikisha kila ofisi ya Serikali inakuwa na miundombinu inayowezesha kuunganishwa kwenye mpango huo wa TEHAMA utakaoongeza tija kiutendaji.