ISHU ya wapenzi zilipendwa, Wema Isaac Sepetu na Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kurudiana inadaiwa kumtesa mpenzi wa sasa wa
Diamond ambaye ni mtangazaji wa DTV, VJ Penniel Mungilwa ‘Penny’ hivyo
kulazimika kukiri kuwa hajawahi kupitia wakati mgumu kama anaopitia
sasa.
“Watu wanapomwambia au kumuuliza Penny habari za Diamond kurudiana na Wema amekuwa akiumia sema tu watu hawajui,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, baada ya taarifa hizo kuwa habari ya mjini, mwishoni mwa wiki iliyopita, Penny alifunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa anachokifanya ni kuhakikisha anamshikilia staa huyo wa Bongo Fleva hadi hapo Mungu atakapoamua vingine.
“Katika uhusiano niliowahi kuwa nao huu ni mgumu mno,” ilisomeka sehemu ya utetezi wa Penny aliouandika juu ya penzi lake na Diamond.
Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Hakuishia hapo kwani aliendelea kujitetea kwa wadau wake ambao
walimjibu kuwa kinachoonekana anamhofia Wema ambaye akikita penzi lake
kwa Diamond, kwa ustaa wake, atamfanya mwanamuziki huyo kuendelea
kuliweka juu jina lake.Katika maelezo yake, Penny alikiri kuwa mapenzi yanatesa lakini anaamini mateso hayo ni ya muda tu hivyo liwalo na liwe yeye anampenda Diamond.
Wiki iliyopita, Wema na Diamond waliripotiwa wakidaiwa kurejesha upya penzi lao lililozimika mwaka jana, jambo ambalo lilimpa Penny wakati mgumu huku akieleza kuwa anachoamini ni kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa penzi hilo.