Alipofikishwa hospitali madaktari walimueleza wasingeweza kumsaidia sababu kipande cha uume alioukata kiliachwa sehemu ambayo alilifanya tendo hilo, hivyo ikaamuliwa arudi nyumbani kwake akakichukue ili aweze kupata matibabu.
Yang Hu, 26, alifanikiwa kurudi tena hospitali, huku akiwa na watu kadhaa, madaktari walimueleza kwamba kipande kilichokatwa kilipoteza damu nyingi sana hivyo ingeshindikana kuweza kukiunga tena.
Marafiki wa Yang walisema kila kukicha jamaa alikuwa anatingwa sana na mawazo kutokana na ukweli kwamba toka alipohamia jijini hapo hakuwahi kupata demu.
Mbaya zaidi, walisema, jamaa alikuwa akifanya kazi kwa masaa mengi kwenye kiwanda cha nguo ndani ya Jiaxing, kwenye jimbo la Zhejiang Mashariki ya China, huku wakihisi kuwa ndiyo kitu kilichomsababisha kutokuwa na muda wakukutana na mwanamke.
Msongo kichwani ulizidi kuongezeka kwa kasi, kiasi cha kumfanya kuzidi kujisikia vibaya zaidi, mnamo tarehe 27 Oktoba mara baada ya kurudi nyumbani majira ya saa 3 usiku jamaa alikodi chumba na kuamua kuukata uume wake kutokana na kuona kwamba hakikuwa ni kitu cha maama na hakikuwa na faida naye, huku akiamini kitendo hicho kingeweza kumsaidia kuacha kufikiria juu ya maswala ya mademu