Hata hivyo, Mungai ameishauri Serikali kuhakikisha kuwa inapunguza gharama za vibali vya kuwaingiza wageni wanaofanya kazi hasa idara ya elimu ili kutimiza malengo ya matokeo makubwa sasa (Big Result Now).
Mungai alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, katika sherehe za mahafali ya nne ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Ghomme iliyopo nje kidogo ya jiji.
“Siku chache baada ya Serikali kutangaza operesheni ya kuwatimua watu wanaoishi kinyume cha sheria katika baadhi ya mikoa, kuna walimu wameondolewa kwa nguvu tena kwa kutumia vyombo vya dola.
“Wito wangu kwa Serikali ni heri ingetafuta utaratibu mwingine hata ikiwezekana vibali vyao vya kuishi hapa Tanzania kama vimeisha basi viongezwe kwa kuwa mchango wao hasa kwa upande wa elimu ni mkubwa,” alisema.
Alishangaa kuona watu hao wanafukuzwa wakati Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambapo nchi hizo zimekubaliana kushirikiana katika kila nyanja.
“Serikali ihakikishe inazisaidia shule binafsi kwa kuwapatia walimu moja kwa moja toka vyuoni na kuzisaidia endapo misaada itahitajika hasa katika upande wa vifaa vya maabara ili kuimarisha masomo ya Sayansi kwa vijana,” alisema.
Awali akisoma taarifa katika mahafali hayo, Mkuu wa Shule hiyo, Emmanuel Malangalila, alisema jumla ya wanafunzi wanaohitimu ni 62