
MASTAA wetu Bongo ukimtokea ghafla na ukataka kumpiga picha bila
kujiremba unaweza kumuua kwa hofu, siku za karibuni kamera ya FC
ilimkosesha raha nyota wa filamu Swahiliwood Kajala Masanja pale
alipokutana na mpiga picha wetu na kutaka kumpiga picha kama sehemu ya
kumbukumbu katika matukio, msanii huyo alizuia huku akilalamika.

![]() |
Kajala akiwa mtaani akimzuia mpiga picha mahiri wa FC ambaye hayupo pichani, hataki kupigwa picha hajajiandaa kujipiga Make up kuchagua pamba kali. |

“Aaah sitaki jamanii unanipigaji picha hivi hata sijajiandaa jamani, nipo rafu sipendi ukipiga picha angalau uwe smart, usinipige picha sitaki sitaki sijajiandaa picha zitakuwa mbaya please usifanye hivyo,”anasema.
Utafiti unaonyesha kuwa mara nyingi nyota wa filamu wamejenga tabia ya kujiandaa kwa kujipodoa wakiwa wapo location au wakifanya mahojiano na wanahabari, hivyo kuwa na muonekano tofauti na wanavyokuwa na maisha ya kawaida wakiwa katika mishemishe za maisha halisi.