Akichonga na paparazi wetu, Mama Kanumba alisema hivi karibuni kuna filamu imetoka kwa watoto wa baba Kanumba waliopo Shinyanga ambayo imewekwa nembo ya kampuni ya mwanaye, Kanumba The Great Film hivyo haitambui.
“Jamani kampuni ya Kanumba haina tawi Shinyanga kama filamu hiyo inayosambazwa huko bali hiyo imechezwa na watu ambao hawatambuliki katika kampuni ya marehemu mwanangu,” alisema Mama Kanumba.
-GPL