WASHAMBULIAJI Didier Drogba, Salomon
Kalou na Gervinho wote wamefunga leo Ivory Coast ikiifumua 3-1 Senegal
na kuongeza matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwakani.
Drogba alifunga kwa penalti dakika ya
tano, kabla ya winga wa zamani wa Arsenal, Gervinho kufunga la pili
dakika tisa na baadaye kipindi cha pili Salomon Kalou akafunga la tatu
mjini Abidjan.
Bao pekee la Senegal lilifungwa na Papiss Cisse dakika tano kabla ya filimbi ya mwisho.
Tembo wauwaji: Wachezaji wa Ivory Coast wakishangilia ushindi wao leo
Sasa Ivory Coast watahitaji sare au
kufungwa si zaidi ya wastani wa bao moja katika mchezo wa marudiano moja
ili kujikatia tiketi ya Brazil mwakani. Seneal yenyewe itahitaji
kushinda 2-0 tu nyumbani, ili kujihakikishia kurejea Fainali za Kombe la
Dunia.
Didier Drogba ameifungia Ivory Coast leo
Salomon Kalou na Drogba walicheza pamoja Chelsea miaka kadhaa
Umefanya vizuri: Gervinho akizungumza na kocha Sabri Lamouchi baada ya mechi