TIMU
ya taifa ya Ghana imeifunga Misri mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza wa
hatua ya mwisho ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwakani nchini
Brazil.
Mshambuliaji Asamoah Gyan alifunga mabao mawili dakika ya tano na 52, wakati Wael Gomaa alijifunga dakika ya 21.
Amefunga: Asamoah Gyan ameifungia Ghana mabao mawili
Mohamed
Aboutrika aliifungia bao pekee Misri kwa penalti dakika ya 41, kabla ya
Majeed Waris kuifungia Ghana dakika ya 44, Sulley Muntari akafunga kwa
penalti dakika ya 72 na mchezaji mpya wa Chelsea, Christian Atsu
akahitimisha karamu ya mabao ya Ghana dakika ya 87.
Kikosi
cha kilikuwa; Ghana: Dauda, Inkoom, Akaminko, Sumaila, Opare, Essien,
Muntari/Badu dk83, K Asamoah, A Ayew/Atsu dk83, Waris, Gyan/Wakasu dk79.
Misri:
Ekrami/El Shenawy dk57, A Fathi, W Gomaa, Nagieb, Shedid/Shikibala
dk46, Ashour/Mehamadi dk40, Ghaly, El Neny, Aboutrika, W Soliman na M
Salah.
-BIN ZUBEIRY