Like Us On Facebook

Bango linaloonyesha picha ya Yesu akiwa amechorwa Tattoo mwili mzima lawakera wakristo

            Bango linaloonesha picha ya Yesu ikiwa imechorwa tattoo imewakasirisha wakristo waishio Texas Marekani, hasa West Lubbock ambako ndiko bango hilo lilipowekwa.

Mkazi mmoja wa eneo hilo alipoulizwa alisema, “siipendi hiyo picha, naona kama inaonesha dharau.”Mwingine alisema, “mi ninafikiri inakufuru.”


Bango hilo linaonesha picha inayotumika sana kuashirika taswira ya Yesu Kristo, zinaomuonesha akiwa amevaa taji la miiba huku akiwa amechorwa tattoo zilizoandikwa dhambi za wote walioenda kwake na akawasamehe, hivyo wachoraji wanaashiria amebaki nazo na wao wako safi! 


Hata hivyo ,kundi la watu ambao wameweka bango hilo wamelitetea na kudai kwamba wamechora na kuliweka kwa nia nzuri ili kuwahubiri watu waende kwake na kusafishwa dhambi zao.

Bango hilo limeandikwa address ya tovuti ambayo ina video inayoonesha watu wanaenda kwa Yesu na wanasafishwa dhambi zao.


TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari