Like Us On Facebook

ZIJUE KLABU ZA LIGI KUU UINGEREZA ZINAZOSAPOTI USHOGA

          WASIMAMIZI wa LIGI KUU ENGLAND wamesema ni juu ya Klabu zenyewe na Wachezaji wenyewe kuamua kama wataunga mkono Kampeni ya Kutetea Haki za Mashoga kwa kufunga Nyuzi za Rangi ya ‘Upinde wa Mvua’ kwenye Buti zao wakati wa Mechi za Ligi za Wikiendi hii.
Tayari Taasisi ya Hisani ya Mashoga, Stonewall, imetuma Nyuzi hizo spesho kwa Vilabu 92 vya Ligi Kuu England na Klabu za Ligi za Madaraja ya chini na pia Klabu 42 za Soka ya Kulipwa huko Scotland.
Kwenye Kampeni hii, iitwayo The Right Behind Gay Footballers, Wachezaji wataombwa kutumia Nyuzi hizo kwenye Mechi za Septemba 21 na 22.
Lakini Msemaji wa Ligi Kuu England amesema: “Ujumbe wa msingi wa Kampeni hii ni mzuri na ni kweli sisi na Wadau wetu tumeshirikiana na Serikali kuhakikisha Ajenda yote ya Usawa inaeleweka na tunashiriki. Lakini hatukuhusishwa mapema kwenye Kampeni hii. Hivyo ni juu ya Klabu na Wachezaji wenyewe kuamua kama wanaisapoti.”
WACHEZAJI Soka huko England na Scotland wamealikwa kuisaidia Kampeni ya kuunga mkono Mashoga kwa kutakiwa kufunga Nyuzi za Rangi ya ‘Upinde wa Mvua’ kwenye Buti zai wakati wa Mechi za Wikiendi hii inayokuja.
Tayari Taasisi ya Hisani ya Mashoga, Stonewall, imetuma Nyuzi hizo spesho kwa Vilabu 92 vya Ligi Kuu England na Klabu za Ligi za Madaraja ya chini na pia Klabu 42 za Soka ya Kulipwa huko Scotland.
Kwenye Kampeni hii, iitwayo The Right Behind Gay Footballers, Wachezaji wataombwa kutumia Nyuzi hizo kwenye Mechi za Septemba 21 na 22.
KLABU 29 ZINAZOSAPOTI MASHOGA:
-LIGI KUU ENGLAND: Arsenal, Aston Villa, Crystal Palace, Liverpool, Manchester City, Norwich, Sunderland, West Ham, West Brom
-CHAMPIONSHIP: Birmingham, Blackburn, Doncaster, Huddersfield, Ipswich, Leicester, Millwall, Sheffield Wednesday
-LIGI 1: Carlisle, Crewe, Gillingham, Leyton Orient, MK Dons, Peterborough, Preston, Tranmere
-LIGI 2: Bristol Rovers, Exeter, Dagenham & Redbridge, Northampton
LISTI IMEHAKIKIWA TAREHE 18 Machi 2013
Huko Uingereza, haki za Mashoga zinalindwa na hata FA ina msimamo wa kukemea Mashoga kubaguliwa.
Kwa sasa hakuna hata Mchezaji mmoja huko Uingereza alieibuka bayana na kukiri yeye ni Shoga.
Mwaka 1990, Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya England ya U-21 pamoja, Justin Fashanu, alikuwa ni Mchezaji wa kwanza wa Kulipwa kutangaza yeye ni Shoga lakini Mwaka 1998, Fashanu alijiua mwenyewe akiwa na Miaka 37.


TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari