Like Us On Facebook

WIVU WA MAPENZI WASABABISHA MUMEWE NA SHAMSA FORD ASABABISHE TIMBWILI KINONDONI

 
WIVU wa mapenzi umesababisha mume mtarajiwa wa mwigizaji Shamsa Ford, Dickson Matoke aibue timbwili kwa shabiki mmoja aliyekuwa akimpongeza mwigizaji huyo.
Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Mgahawa wa Twiter, Kinondoni jijini Dar wakati mwanaume mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja alipomfuata Shamsa kuonesha upendo, ndipo Dickson alipoibua timbwili.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimvutia waya Shamsa ambaye inasemekana yupo katika mikakati ya kuoana na Dickson, akafunguka:
“Mmepata wapi hizo stori? Kweli nyie ni noma,  haikuwa ishu kubwa sana, yaliisha jamani,” alisema Shamsa.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari