Wagonjwa wengi wanaokabiliwa na maradhi ya baridi yabisi wameacha kutumia vidonge ambavyo wamekuwa wakipewa mahospitalini na badala yake wameanza kutumia mafuta hayo kupanga sehemu za maungio ya mwili kwa kuwa
wanapata ahueni ya haraka.
Watu wengi wa umri wa makamo wamekuwa vinara wa kuchukua kondomu ambazo zinasambazwa bure nchini Afrika Kusini kutokana na nchi hiyo kuwa na maambukizi makubwa ya magonjwa ya ngono na virusi vya UKIMWI lakini matumizi yake yamekuwa si ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo tena.
Utafiti uliofanyika huko Soweto umethibitsha watu wengi wa makamo wanatumia zaidi mafuta hayo katika kupambana na maumivu yanayochangiwa na baridi yabisi ambayo imekuwa ikiwasumbua mno watu wenye umri mkubwa.
Wazee wengi wamesema kutokana na kupatikana kwa urahisi kwa kondomu kwao imekuwa ni kitu cha faraja kwa sababu wameweza kupata tiba mbadala ya kupaka kwenye maungio mwilini badala ya kuendelea kunywa dawa kila siku.