Like Us On Facebook

VIDEO:SHABIKI WA KIUME AKIWA KIFUA WAZI AMRUKIA BEYONCE NA KUMKUMBATIA NA AKIJARIBU KUMVUTA KUTOKA JUKWAANI

                    Mama Blue Ivy Beyonce Knowles amekutana na ‘kisanga’ cha aina yake jumapili (September 15), alipokuwa akiperfom jukwaani nchini Brazil wakati akiimba hit yake ya ‘Irreplaceable’ na kujaribu kushow love kwa fans wake walio karibu na jukwaa kwa kuwashika mikono.
Shabiki mmoja wa kiume akiwa kifua wazi aliona mapenzi yamezidi kiwango na isitoshe ndio nafasi yenyewe hii ya kumgusa super star anaemkubali (kama alivyofanya shabiki wa Shilole katika Serengeti Fiesta ya Dodoma), kwa mzuka binafsi alimrukia ghafla Beyonce na kumkumbatia akimvuta kutoka jukwaani, lakini mlinzi aliyekuwa karibu alimuokoa mwimbaji huyo na kumvuta haraka kurudi jukwaani.
Uzoefu katika kila kitu una faida yake, Beyonce aliendelea na show bila kupoteza dakika kama vile hakuna kilichotokea pale jukwaani. Utu uzima dawa, member huyo wa Destiny’s Child alionesha busara yake baada ya kumaliza kuimba wimbo huo alimfuata shabiki huyo na kupiga nae story akimwambia kila kitu kiko poa, akauliza jina na kumwambia anampenda pia. “It’s alright, it’s alright, What’s your name?…Thank you, I love You too”.
Alisikika Beyonce akipiga story na shabiki huyo huku akishangiliwa na umati uliohudhuria.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari