WAKALI wa soka ya kitabuni England, Swansea wameanza vyema Europa League baada ya kuifumua mabao 3-0 nyumbani kwake Valencia iliyomaliza na wachezaji 10.
Wenyeji walilazimika kucheza 10 kwa takriban dakika 80, baada ya beki Adil Rami kutolewa nje kwa kadi nyekundu, kufuatia kumchezea rafu Wilfried Bony.
Mshambuliaji huyo ndiye aliyeifungia Swansea bao la kwanza dakika ya 14 usiku huu, hilo likiwa bao lake la tano katika mechi nanemsimu huu.
Mabao mengine yalifungwa na Michu dakika ya 58 na Jonathan de Guzman dakika ya 62.
Kikosi cha Valencia kilikuwa: Guaita, Barragan, Rami, Feghouli/Pabon dk59, Mathieu, Ever/Costa dk14, Javi Fuego, Guardado, Canales/Bernat dk66, Cartabia na Postiga.
Swansea: Vorm, Rangel/Davies dk56, Amat, Chico, Tiendalli, de Guzman, Canas, Pozuelo, Dyer/Lamah dk65, Michu/Shelvey dk77 na Bony.
Kitu hicho: Wilfried Bony akiifungia bao la kwanza Swansea dhidi ya Valencia
Nenda Nje: Adil Rami akionyeshwa kadi nyekundu
Pati la ushindi: Swansea wakishangilia baada ya Wilfried Bony kufunga
Katika mchezo mwingine, mabao mawili ya Jermain Defoe yalichgia ushindi wa 3-0 kwa Tottenham dhidi ya Tromso, bao lingine akifunga Christian Eriksen .
Pamoja na ushindi huo, Mousa Dembele, Danny Rose and Younes Kaboul wote walitoewa nje baada ya kuumia.
Tottenham ilimaliza mechi na wachezaji 10 kutokana na Kaboul kutolewa nje baada ya kuumia, wakati kocha Andre Villas-Boas amemaliza idadi ya wachezaji wa kubadili.
Spurs: Lloris, Naughton, Kaboul, Dawson, Rose, Sandro, Dembele, Sigurdsson, Holtby, Lamela na Defoe.
Tromso: Sahlman, Kristiansen, Fojut, Koppinen, Causevic, Bendiksen, Johansen, Drage, Pritchard, Moldskred, Ondrasek.
Mfalme wa mabao: Jermain Defoe ameifungia mabao mawili Spurs
Safi hiyo: Defoe akimtungua kipa wa Tromso, Marcus Sahlman kufunga la kwanza
Michael Dawson akigombea mpira na Josh Pritchard wa Tromso
La pili kiulaini: Defoe akifunga bao tamu
Ruka juu: Defoe akishangilia na Lewis Holtby baada ya kufunga