Like Us On Facebook

RADO:"BONGO MOVIE HAWANA MSAADA WOWOTE, WANASUBIRI MSANII AFARIKI NDIPO WAONEKANE".

Simon Mwapagata.
                                   Rado mwigizaji wa filamu Bongo
MSANII wa filamu na mtayarishaji pia wa filamu Bongo Simon Mwakipagata ‘Rado’ amelishutumu na kulilaumu kundi la filamu la Bongo Movie Unity kwa kukosa upendo na kushindwa kusaidia katika matatizo, Rado aliyasema hayo kufuatia hivi karibuni kupata ajali ya gari na kujikuta akijiuguza pekee yake bila kupata faraja kutoka kundi hilo wakati yeye ni katibu wa kundi hilo.
.


Simon Mwakipagata
Rado akiwa katika suti ya maana .

Simon Mwapagata
RADO maarufu kama Baba Mage akiwa katika pozi la picha.
Siku zote mimi upenda kuwa mkweli hata kama mwingine atachukia hivi karibuni wakati narudi kutoka Location nilipata ajali na kuumia sehemu ya kifua ilikuwa ni ajali mbaya namshukru Mungu kuniponya lakini rafiki zangu wa Bongo movie hakuna hata mmoja aliyejitokeza kunijulia hali wakati walikuwa na taarifa, lakini tu hao hao wangesikia nimekufa wangekuwa wa kwanza kuunda kamati ya mazishi,”anasema Rado.
Msanii huyo nyota anadai kuwa tukio hilo ni la pili kwake kupata ajali lakini mara zote hizo amekuwa jirani na wasanii ambao alikuwa akiigiza nao katika kundi la Jumba la Dhahabu ambao ni Niva, Baga, Wema Sepetu na wasanii wengine ambao kila awapo na tatizo uwa mbele katika kumsaidia na kumfariji katika ugonjwa lakini si kundi ambalo yeye ni kiongozi pia kama katibu.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari