Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mara Ferdinand Mtui alisema mnamo septemba 17mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika maeneo ya Rwamlimi mjini hapa marehemu alichomwa kisu na kijana mwenzake na kujeruhiwa vibaya sehemu ya ubavuni upande wa kulia hali iliyompelekea kuvuja damu nyingi na kupelekea kupoteza maisha akiwa kwenye matibabu.
Alisema baada ya kujeruhiwa alifikishwa kituo cha polisi na kupewa PF.3. lakini ilipotimu majira ya saa mbili usiku alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Mara.
Kamanda Mtui alisema chanzo cha tukio hilo bado alijafahamika na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo,na kusisitiza kuwa jeshi la polisi linaendelea kumsaka mtu aliyehusika na tukio hilo na mara atakapopatikana atafikishwa katika vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zaidi
Mtui alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za siri kwa jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo ili kuweza kufanikisha kukamatwa wale wote waliohusika na kuwatakawanafunzi pale wanapoona viashilia vya kutisha uhai kujiepusha kwa kukaa mbali na kutoa taarifa jeshi la polisi kama kuna mtu ama watu wanaotishia uhai.