Like Us On Facebook

MAAJABU YA MTI WA MUAROBAINI

               BILA shaka watu wengi wanaujua mti huu lakini naamini wachache ndiyo wanaijua historia yake. Muarobani ulipandwa nchini kwa amri ya Kanali Yusuf Makamba, ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo.
Mzee Makamba aliileta mbegu hii kutoka nchini India na kuipandikiza kijeshi-jeshi katika kaya mbalimbali nchini.
Nchini India, Muarobaini unajulikana kama Village Pharmacy. Watu wengi nchini Tanzania wanaujua mti huu kutokana na sifa yake kubwa ya kutibu ugonjwa wa malaria. Lakini katika makala ya leo utajifunza kuwa mti huu siyo tu unatibu malaria, bali hata magonjwa mengine sugu.

MAGONJWA YANAYOWEZA KUTIBIWA
Unywaji wa juisi ya Muarobaini umethibitishwa na vyuo vikuu vya tiba duniani kuwa una uwezo wa kutoa nafuu kwa watu wenye maambukizi ya HIV na pengine kutibu kabisa magonjwa sugu yanayowasumbua kwa sababu ya kushuka kwa kinga ya mwili.
Muarobaini una uwezo mkubwa wa kuzuia na kutibu ‘allergy’ (mzio) za aina tofauti kwa kupaka juisi yake mwilini na kwa kuinywa.
Huko Marekani na India, muarobaini umeonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia nyani dume kutoa mbegu za uzazi kwa majike na umegundulika kuwa juisi yake inamfaa mwanaume anayetaka kupanga uzazi bila kwenda hospitali kufanyiwa upasuaji mdogo wa kukinga uzalishaji wa mbegu za uzazi (Vasectomy).
Muarobaini pia ni kiboko kwa wanawake wasio na mpango wa kushika mimba. Juisi yake ikipakwa sehemu ya via vya uzazi kwa mwanamke itamsaidia kutopata mimba zisizotarajiwa.
Muarobaini una uwezo mkubwa wa kupambana na kansa na hata kinga ya mwili pia. Tindikali ziitwazo ‘Polysaccharides’ na ‘limonoids’ zilizomo katika magamba, majani na mizizi huboresha kinga ya mwili haraka mno ili kupambana na maradhi kama kansa na mengineyo bila uharibifu wa mwili kama zilivyo dawa zingine za hospitalini.
Muarobaini hutibu kisukari kwa haraka sana. Majani matatu tu ya muarobaini ni dozi tosha kwa mgonjwa wa kisukari na akizidisha anaweza kurudi hospitali na kuwaomba madaktari waitafute sukari kwenye damu yake kwa tochi!
Muarobaini hushambulia wadudu wote wanaoshambulia ngozi ya binadamu kwa usahihi kabisa. Muarobaini hutibu mapunye, mba, ukurutu, upele na magonjwa kadhaa ya ngozi bila madhara yoyote.
Muarobaini hutibu magonjwa ya moyo. Huifanya damu kuwa nyepesi na itembee kwenye mishipa kwa mwendo sahihi na kuyafanya mapigo ya moyo kuwa tulivu kwa wenye maradhi ya moyo.
Ujerumani ambayo ni nchi ya baridi kwa kipindi kirefu cha mwaka, watu hufa kwa mafua tu. Tafiti walizofanya zinasema juisi ya muarobaini hukata mafua haraka zaidi ya dawa yoyote ya hospitalini huku ikikuhakikishia usalama bila madhara.
Muarobaini unaua fangasi. Inawezekana una fangasi miguuni, kwenye maungio ya siri kama mapajani, kwapani, sehemu za siri n.k. tumia juisi ya muarobaini ujipake sehemu zilizoathirika kupambana na fangasi hao bila madhara.
Muarobaini pia ni dawa ya kufukuza wadudu bila madhara ya kemikali. Jaribu kulala chini ya muarobaini lakini angalia pawe na majani yake hapo chini halafu utaona hakuna usumbufu wa mbu wala nzi maana mwarobaini hufukuza wadudu aina kadhaa akiwemo mbu.
Mchanganyiko maalum wa majani ya muarobaini uitwao kwa kitaalam “irodin A” ni sumu ya kuzuia na kutibu malaria. Majaribio mengi yamefanyika hata hapa nchini na muarobaini umeonekana una nguvu ya kupambana na malaria.
Kutokana na uhaba wa nafasi, ningependa kutoa maelekezo kwa msomaji kwa njia ya simu kwa kila tatizo alilonalo kwa kutumia namba ifuatayo. Asanteni kwa kunisoma na tuuenzi muarobaini….

-gpl
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari