Like Us On Facebook

KIUNGO KISHETI PHILIPE COUTINHO KURUDI DIMBANI MAPEMA ZAIDI,NI BAADA YA KUFANYIWA OPERASHENI YA BEGA



 Kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho amesema kuwa matibabu yake ya bega yalifanikiwa vizuri na ana matumaini ya kurudi uwanjani mapema iwezekanavyo.
Coutinho aliumia mwanzoni mwa mwezi huu walipocheza na Swansea na alihitaji kufanyiwa oparesheni ili kumtibu majeraha yake.
Mbrazil huyo alianza vizuri sana msimu huu akiwa na klabu yake ya Liverpool na kukosekana kwake kumeonyesha mapungufu makubwa katika klabu hiyo ya Anfield hasa katika mchezo waliofungwa wikiendi bao 1-0 dhidi ya Southampton.
Nyota huyo kabla hajafanyiwa matibabu ilisemekana atauguza majeraha kwa wiki sita hivyo alitakiwa kukaa nje ya uwanja mpaka mwishoni mwa mwezi Oktoba.Lakini huenda akarudi mapema zaidi.
Coutinho alisisitiza kuwa inaumiza sana kupata majeraha hasa ukiwa katika kiwango kizuri lakini akadai kuwa huwa inatokea kwa mchezaji huku akisema kwa sasa anajitahidi kurudi katika hali yake ya kawaida ili arudi kuisaidia Liverpool katika michezo ya Ligi.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari